GOOD HOPE SUPPORT ORGANIZATION (tafsiri: Shirika la msaada Tumaini Jema) lilifungua milango yake mwezi wa Oktoba 2011, na Januari 2013 shirika likasajiliwa kama shirika la msaada lisilo tengeneza faida (NPO) na lisilo la serekali (NGO) nchini Tanzania.

GOOD HOPE ni shirika la kijamii lilopo katika mkoa Kilimanjaro, wilaya ya Moshi manispaa, kata ya Njoro, mtaa wa sokoni. Moshi inapatikana kwenye kitovu cha mkoa wa Kilimanjaro, na Njoro ni moja wapo ya kata duni katika Manispaa ya Moshi.

Elimu ni sehemu muhimu ya kazi za GOOD HOPE ambazo hutoa katika jamii, na kazi zake zimezingatia katika nguzo tatu:

1 . Mpango wa elimu bure kwa miaka miwili kwa maandalizi ya elimu ya upili/secondary na mpango wa vijana mchana katika kituo chetu.

2 . Mpango wa udhamini kwa wanafunzi wa shule ya sekondari (kidato cha 1 hadi kidato cha 6), chuo kikuu, college, na mafunzo ya ufundi stadi za kazi

3 . Mpango wa uwezeshaji wa mabinti katika kituo chetu cha vijana na katika shule za serikali.

Lengo kuu la GOOD HOPE ni kusaidia wanafunzi wa Moshi na mitaa yake wanaoishi kwenye mazingira magumu, kuanzia wanapomaliza elimu yao ya msingi moja kwa moja hadi chuo kikuu au mafunzo ya ufundi stadi.

Shirika la GOOD HOPE linalenga vijana waliopo katika mazingira magumu, kwa kuwapa ujuzi na elimu muhimu kwa ajili ya maisha yao ya baadae, na familia zao wakati wakijipatia taaluma kwa ajili ya malengo yao. Wanafunzi wanaoishi katika familia zenye matatizo ya kiuchumi au wenye matatizo ya kiafya mara nyingi wana nafasi finyu ya kuendelea na elimu ya juu, lakini GOOD HOPE imekuwa kama daraja la kuwavusha, wanafunzi wetu wanaonyesha uwezo wa kuhifadhi na kufanya tofauti katika jamii zao na maisha yao.

Sera ya GOOD HOPE ni kwa wote halina mrengo wa kidini au wa kisiasa. Tunawapokea wanafunzi wa aina yote bila ya ubaguzi.